Sunday, September 9, 2012

BAADA YA SAUT NA CBE CHUO KIKUU CHA MT. JOHN (SJUT) NACHO CHAPIGA MARUFUKU MAVAZI YASIYO YA MAADILI KWA WAFANYAKAZI NA WANAFUNZI


Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John wenye makao makuu mjini Dodoma umetoa taarifa kupitia website yake juu ya utekelezaji wa sheria ya mavazi itakayoanza kufanya kazi rasmi tarehe 1 Oktoba, 2012. Waraka huo ulioandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Fedha (DVCPFA) unawataka wafanyakazi na wanafunzii wote wa Chuo hicho kufuata muongozo mpya juu ya kanuni za mavazi wanayotakiwa kuvaa pindi wawapo katika majukumu yao chuoni hapo.
Chuo kimeweka Kanuni za mavazi kwa ajili ya watu wote wafanyakazi na wanafunzi. Ninaandika barua hii kuamrisha watu wote kwa usawa kabisa kutekeleza agizo la kuvaa mavazi yanayoendana na maadali ambayo itaanza rasmi tarehe 1 Oktoba, 2012. Nina matumaini, kutokana na kuwa wazi kwa muongozo wa chuo juu ya maadali na madhumuni ya chuo. Kila mwanajumuiya wa SJUT tunategemea ushirikiano wake katika tekelazaji wa agizo hili kwa maadili ya kiroho”, ilisema barua hiyo.
Jengo la Utawala, Chuo Kikuu cha Mt. John, Dodoma.
SJUT si chuo cha kwanza Tanzania kuweka kanuni za mavazi yanayoendana na Maadili ya kiroho na kitanzania, Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) nacho kilitoa muongozo kama huu kwa jumuiya yake, lakini pia baadae Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) nacho kikatoa muongozo kama huo.

Hii imekuja kufuatia na kuporomoka kwa maadili kwa wanafunzi na hata wafanyakazi wa vyuo vikuu juu ya mavazi yanayovaliwa na baadhi yao wakati wa masomo. Mavazi hayo yamekuwa kero ka uongozi wa vyuo, walimu na hata baadhi ya wanafunzi pamoja na wanajamii wanao vizunguka vyuo hivi.

Soma waraka huo wa Chuo hapo Chini....

TO: The SJUT Community of:

(a) Members of staff,

(b) All students.

FROM: DVCPFA – Dodoma

DATE: 7
th September, 2012

CC: The Chancellor

: The Chairman of Council

: Members of the Council

: The Vice Chancellor

: The University Chaplain

: DVCA

: Faculty/School Deans, Associate Deans

: Dean of Students

: Directors

- QAB

- St. Marks’ Centre

- Msalato Centre

- Town Centre

- Postgraduate Studies

- Undergraduate studies

: Heads of Departments

: Chief Security Officer

: President of SOSJUT

: Vice Presidents of SOSJUT

RE: IMPLEMENTATION OF THE SJUT DRESS CODE

The University has put in place a SJUT Dress Code for both staff and students. I am
writing to commit you all to your unequivocal implementation of the code which goes
operational on 1st October, 2012. I am hopeful, with the clear preamble to the code as to
its purpose; every member of SJUT will diligently execute it with full support to both the
letter and the spirit of the code.
The SJUT Dress Code is on SJUT website.
May the Almighty God bless you

 

No comments:

Post a Comment