Thursday, September 13, 2012

KUTOKA UDOM: CHUO KIKUU CHA DODOMA CHATOA MSAMAHA KWA WANAFUNZI 15 WALIOJIHUSISHA NA MGOMO MWEZI JUNI 2011


Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma umetoa taarifa kupitia mtandao wake juu ya kuwasamehe baadhi ya wanafunzi wake 15 waliojihusisha na mgomo wa mwezi Juni, 2011 na kuwaruhusu kufanya mitihani ya ziada badda ya kukosa mitiani yao iliyopita.

Kupitia taarifa hiyo chuo hicho kimesema kwamba, Chuo kimepitisha uamuzi unaoenda pamoja na onyo kali kwa wanafunzi hao 15 kufuatia ushiriki wao katika mgomo wa Juni, 2011 katika Chuo cha Syansi ya Jamii (CHSS) na Chuo cha Sayansi ya Asili na Hisabati (CNMS) katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Aidha katika siku zijazo, mwanafunzi atakaehusika katika shughuli za uvunjifu wa amani chuoni hapo, atajisababishia mwenyewe kusimamishwa masomo na kusababisha adhabu ya haraka bila ya onyo lolote zaidi, ilisema taarifa hiyo.

Taarifa iliwataka wanafunzi walio katika orodha hiyo kuripoti Chuo Kikuu cha Dodoma tarehe 13 Oktoba, 2012 na 14 Oktoba, 2012 kwani mitihani hiyo ya mwisho itaanza Jumatatu ya tarehe 15 Oktoba, 2012.
Wanafunzi waliotajwa wamerejeshwa na masharti yafuatayo:
  • Wanatakiwa kulipa ada yote ya masomo na ada nyengine za chuo (Gharama za Moja kwa moja) kabla ya septemba 15, 2012
a)  Gharama za moja kwa moja (Direct Cost): CRDB Namba ya Akaunti 01J1083343300
b)  Ada (Tuition Fee): CRDB Namba ya Akaunti 01J1082344900
  • Wanatakiwa pia kulipa ada 10,000/= ya kusajiliwa tena: CRDB Namba ya Akaunti 01J1083343300
  • Wanatakiwa kula kiapo mbele ya kamishna wa Viapo na kusema kwamba hawatojihusisha katika kitendo chochote ambacho ni kinyume cha sheria na taratibu (Students By-Law) za Chuo Kikuu cha Dodoma. Kiapo hicho kitatolewa wakati wa usajili katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Ilisema taarifa hiyo..
MAJINA YA WANAFUNZI HAO.

 

No comments:

Post a Comment