Friday, September 7, 2012

MAKALA YA VYUO: FAHAMU HISTORIA YA CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA HUBERT KAIRUKI, Je? WAJUA KWAMBA NDIO CHUO CHA KWANZA BINAFSI KUPATA HADHI YA KUWA CHUO KIKUU TANZANIA.


Leo tunaanza kukichambua Chuo Kikuu Cha kumbukumbu Cha Hubert Kairuki katika mfululizo wa makala zitakazokuwa zinakujia kila Ijumaa kuhusu Historia za Vyuo vikuu vyetu nchini Tanzania.
Prof. Hubert Kairuki
Muasisi wa HKMU
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Habert Kairuki (HKMU) ni moja kati ya vyuo vikuu vikubwa nchini Tanzania, ambacho ndio chuo kikuu cha kwanza binafsi Tanzania kupata hadhi ya kuwa chuo kikuu, makao yake makuu yapo jijini Dar es salaam, Chuo hiki kinachofundisha fani mbalimbali za maswala ya Sayansi za Tiba tu kwa sasa.
Historia ya Chuo hiki ilianza mwaka ya 1997 chini ya Mtandao wa Afya na Elimu (The Mission Mikocheni Health AND Education Network (MMHEN)). Awali (HKMU) kilikuwa kikijulikana kama Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Mikocheni (Mikocheni Intenational University (MIU)). Muasisi wa Chuo hiki ni hayati Prof. Hubert Kairuki ambae alikuwa ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Hubert Kairuki alifariki mwaka 1999. Makamu mkuu wa pili aliyechukua nafasi ya Prof. Kairuki alikuwa ni Prof. Esther Mwaikambo. Kwa sasa Chuo hiki kipo chini ya Makamu Mkuu wa Chuo wake Prof. Keto Mshigeni ambae ni mtaalamu maarufu duniani katika maswala ya kisayansi.
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki ndio chuo cha Kwanza binafsi Tanzania kupata hadhi ya kuwa Chuo Kikuu kupitia Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) mwezi Juni, 2000. HKMU pia kinatambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), na pia kipo katika Muongozo wa Elimu ya Tiba wa Kimatifa (IMED). Ambapo HKMU inajivunia kwa kuwa na Vifaa bora na vya kisasa kwa ajili ya kufundishia na utafiti, maktaba yenye vitabu na yenye muongozo wa kutumia kompyuta pamoja na huduma ya mtandao muda wote mwanafunzi awapo chuoni.
Mrs. Kokushubila Kairuki,
Mwenyekiti
 Bodi ya Wadhamini

Kwa sasa HKMU kinatoa masomo katika fani ya sayansi ya Afya tu, lakini mpango wa chuo ni kutanua wigo wa elimu kwa kuanzisha masomo ya fani za sayansi na za kijamii. Kozi zinazofundishwa kwa sasa ni Doctor of Medicine (MD), Shahada ya kwanza ya Uuguzi (BScN), Diploma ya Uuguzi, na Cheti katika fani ya Wholistic Therapeutic Counseling pamoja na kozi za awali zakuingia chuo kikuu (Pre-University Entry Programme).
HKMU pia kinatoa mafunzo katika Postgraduate Diploma in Obstetrics and Gynecology, Postgraduate Diploma in Paediatrics and Child Health, pamoja na Master of Medicine (M.Med). Pia kuna kozi katika fani za Internal Medicine, Surgery, Obstetrics na Gynecology, Pediatrics na Child Health.
HKMU kwa mara ya kwanza kilifungua milango yake kwa umma mnamo tarehe 27 Agosti, 1997 kama chuo kidogo lakini makini kilichojikita kutoa mafunzo kama chuo binafsi, dhamira yake ikiwa ni kutoa wataalamu wa fani ya tiba za afya. Kwa muda huo sababu kubwa ya kuanzishwa chuo hiki ni kupunguza upungufu wa wataalamu wa afya nchini Tanzania kwa kufundisha madaktari na wauguzi katika ngazi ya cheti, diploma, shahada na stashahada. 

Prof. Fredrick Kaijage,
Mwenyekiti
Baraza la Chuo

Tangu Tanzania inapata uhuru, Afya, Umasikini na Ujinga ndio vitu vilivyokuwa maadaui wa Taifa hili, lakini Serikali pamoja na asasi za kijamii pamoja na Taasisi za kimataifa hawakuweza kufikia malengo katika kupambana na matatizo hayo makubwa ya Taifa hili. Watanzania wengi walidharau majanga haya yanayoikumba Taifa lakini watu wachache hasa wasomi na taasisi za kiafya zilizoanzishwa walichukua hatua za kimatendo kutatua Matatizo hayo.   
Moja ya wasomi alikuwa ni Hayati Prof. Hubert C.M Kairuki ambae kabla ya HKMU kuanzishwa alikuwa ni mhadhiri katika Kitivo cha Tiba, Chuo kikuu cha Dar es salaam. Nia yake ilionekana mwaka 1991 katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Tiba Tanzania (MAT) baada ya kualikwa kama Mgeni Mkufunzi, alichukulia fursa hiyo kama sehemu ya kuelezea mawazo yake juu ya matatizo yanayotukabili kama Taifa na pia kueleza hatua za kuchukua kama wasomi katika kulinusuru Taifa juu ya matatizo hayo. Moja ni kuelezea juu ya  upungufu mkubwa wa mafunzo ya Udaktari wa tiba Tanzania..

Prof. Keto Elitabu Mshigeni
Makamu Mkuu
 HKMU

Kwa wakati huo akiwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mikocheni, Prof. Kairuki alipenda kufanya vitu kwa matendo hivyo alianza maandalizi ya kuanzisha shule ya tiba katika hospitali yake ya Mikocheni (MMH), Dar es salaam. Na mwaka 1992 katika sherehe ya kuadhimisha miaka mitano ya Mission Mikocheni Hospital (MMH), Prof. Kairuki alitangaza mipango ya ya Kuanzisha Chuo kikuu kitakachojulikana kama Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Siyansi ya Tiba cha Mikocheni (MIUHS).
Lakini baadae Prof. Kairuki alitaka Chuo hiki kisiwe kinatoa masomo ya Siyansi ya Tiba pekee, hatua iliyopelekea kubadilishwa jina kwa MIUHS na kusajiliwa kwa jina la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Mikocheni (MIU). Baadae katika kuonyesha umuhimu wake na kutoa heshima kwa muasisi wa Chuo hiki, uongozi wa chuo hiki uliamua kubadisha jina na Kukiita Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) Februari, 1999.

Prof. Paschalis G.N. Rugarabamu
Makamu Mkuu Msaidizi
Taaluma
HKMU

Tayari wanafunzi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Zambia, Namibia, Uingereza na Nigeria wamesha hitimu fani mbalimbali kutoka HKMU. Dhamira za Chuo hiki kwa siku za karibuni ni kutanua uwigo wa fani kwa kuanzisha masomo ya fani mbalimbali kwa siku za hivi karibuni ili kutimiza malengo ya Chuo hiki ya kuwa mfano wa kuigwa kwa vyuo vingine Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kutoa elimu ya kiwango cha juu, Tafiti za kina na kuwa mfano katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Chuo hiki kipo eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam kiwanja namba 322, Regent Estate, Barabara za Ali Hassan Mwinyi na Old Bagamoyo, Kilometa 7 kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam. Ukiacha kuwa karibu kabisa na fukwe za bahari ya Hindi na Hoteli kubwa za kitalii, chuo hiki pia kipo karibu kabisa na vivutio vingine vya kiutalii nchini Tanzania.
Uongozi Pamoja na Wahadhiri wa HKMU katika moja ya Mahafali ya Chuo hiko.
The Hubert Kairuki Memorial University
P.O. Box 65300, Dar Es Salaam, Tanzania.

Physical Address:
Plot. No. 322 Regent Estate, Dar Es Salaam
6 th Floor MMHEN building

Tel.: +255-22-2700021 /4 ext 282 or 276 | Fax: +255-22-2775591
Email:
info@hkmu.ac.tz ; v_c@hkmu.ac.tz ; secvc@hkmu.ac.tz
 

 

No comments:

Post a Comment