Sunday, September 16, 2012

MISS EXCELLENCE CHUO KIKUU HURIA TANZANIA 2012: HATIMAYE ZUENA NASEEB AVISHWA TAJI LA MISS EXCELLENCE OUT 2012

 
Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha kwa mlimbwende Zuwena Naseeb baada ya kuibika mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Excellence wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) 2012, akiwabwaga wenzake tisa na kujinyakulia Kitita cha Shilingi 6,030,000 itakayomuwezesha kusoma Shahada ya Pili (Masters) katika Chuo Kikuu Huria Tanzania, shindano lililofanyika katika ukumbi wa Mwinyi uliopo kinondoni Biafra na kuhudhuriwa na watu na wadau mbalimbali wa maswala ya urembo.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa Naima Julius na nafasi ya tatu alinyakuliwa na mrembo Tela Alestas. Ambapo Mgeni rasmi katika shindano hilo la warembo wa OUT alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mh. William Lukuvi, ambae alimpongeza mrembo huyo kwa kuibuka mrembo lakini alimtaka kuchukua nafsi hiyo kukitangaza Chuo hicho na atumie nafasi aliyoipata ya kusoma Shahada ya pili vizuri ili kuja kuisaidia jamii yake na Taifa kwa ujumla.

Shindano hilo lililohudhuria pia na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Prof. Tolly Mbwete ambae alipata nafasi ya kuongea maneno machache, akianza kwa kumpongeza mshindi wa shindano hilo alimtaka atumie nafasi hiyo vizuri ikiwa pamoja na kukitangaza chuo. Makamu Mkuu huyo pia aliwapongeza waandaji na majaji wa shindano hilo kwa kufanikisha kufana kwake kwani hiyo imetokana na kazi yao nzuri.  

Katika pambano hilo la kila mwaka lililoshirikisha warembo kumi wa kutoka chuo hicho, upande wa burudani Banana Band chini ya Banana Ally Zoro alisimamia kuhakikisha wanaz ikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo. Kwa mwaka jana taji hilo la Miss Excellence OUT lilikwenda kwa Neema Mtitu ambae usiku wa jana alirithisha taji hilo kwa Miss Zuena Naseeb.


Tanzania Campus Vibe inapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Majaji kwa kazi kubwa na ngumu waliyoifanya na Pia kamati ya shidano hilo mwaka huu kwa kufanikisha kufana kwake. Pia tunapenda kuwapongeza warembo wote walioshiriki na kwa pekee Miss Excellence 2012, Zuena Naseeb. Mwisho kabisa pongezi zetu zinaenda kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa juhudi zake za kuendeleza vipaji vya vijana chuoni hapo.

Mshindi wa Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb (aliyekaa) mara baada ya kuveshwa taji lake la umalkia wa shindano hilo mwaka huu, Kulia Ni mshindi wa pili Naima Julius na kushoto ni Mshindi wa tatu Tela Alestas
 
Miss Excellence OUT 2011, Neema Mtitu (gauni la njano) akimkabidhi shada la maua Miss Excellence OUT 2012 Zuena Naseeb hapo jana usiku mara ya baada ya kutangazwa mshindi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mh. William Lukuvi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi 6,030,000 mshindi wa shindano la Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb, pesa ambayo itamuwezesha kusoma shahada ya pili (Master) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwete
   
Mgeni rsami Mh. William Lukuvi, Makamu Mkuu wa Chuo, Miss Excellence 2011 pamoja na warembo hao mshindi wa kwanza mpaka wa tano mara baada ya kukabidhi zawadi


Majaji wa shindano la Miss Excellence OUT 2012 wakifuatilia kwa makini shindano hilo usiku wa kumakia leo

Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora mara baada ya mchujo kufanyika
 
Burudani ya nguvu ilitolewa na warembo wote walioshiriki katika shindano hili, huu ulikuwa ni wimbo wa Bob Junior ujulikanao kama Nichum
 
Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb akiwa katika vazi lake la ufukweni
 
Mshindi wa pili wa shindano la Miss Excellence OUT 2012, Naima Julius ukionyesha vazi la ubunifu
 
Banana Ally Zoro akifanya makamuzi na bendi yake ya Banana Band

No comments:

Post a Comment